1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya raia 9,000 wa DRC waingia Burundi

29 Januari 2018

Zaidi ya raia 9,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamekimbilia Burundi kutoka eneo la Fizi lililoko mashariki mwa Kongo. Wakimbizi hao wanasema kuwa wanakimbia mapambano kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa Maimai. Wakimbizi hao wamesema kwamba hadi sasa hawajapata msaada wowote tangu walipowasili wiki tatu zilizopita.

https://p.dw.com/p/2riN6

Aidha, wakimbizi hao wanatakiwa kwenda katika kambi zilizoko kwenye mikoa iliyo mbali na maeneo nayopakana na Kongo kama inavyoagiza sehria ya kimataifa kuhusu masuala ya wakimbizi.

Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Amida Issa kutoka Bujumbura, Burundi.