1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy amesema Bakhmut bado inadhibitiwa na Ukraine

21 Mei 2023

Rais wa Urusi, Vladmir Putin leo Jumapili amewapongeza wapiganaji mamluki wa kampuni binafsi ya Wagner na jeshi la Urusi kwa kile alichokiita kuwa ni ukomboziwa mji ulio mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4Rd5G
G7 Gipfel in Japan, Hiroshima | Joko Widodo und Wolodymyr Selenskyj
Picha: Secretary President of Indonesia/Handout/AA/picture alliance

Katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye tovuti ya ikulu ya Kremlin, Putin amesema kuwa mapambano ya muda mrefu yaliyogubikwa na umwagaji damu mkubwa kwa takribani miezi 15 yameisha kwa kuipa Urusi ushindi. Ameongeza kuwa wote walioshiriki vyema upande wa Urusi watapewa tuzo za kitaifa. Licha ya pongezi hizo za Putin na kuutambua ushindi wa Urusi mjini Bakhmut, Ukraine imejibu kwamba bado inapigania kupata udhibiti wa mji huo. Msemaji wa Rais Volodymyr Zelensky mapema leo alikanusha taarifa kuwa Rais huyo wa Ukraine amethibitisha kwamba Urusi inaidhibiti Bakhmut alipokuwa akizungumza na Rais Joe Biden kabla ya kuanza kwa mkutano wa kundi la mataifa tajiri la G7 wa leo mjini Hiroshima, Japan.