1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky anatazamiwa kukutana na Kansela Olaf Scholz

Sylvia Mwehozi
6 Septemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kukutana hii leo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Frankfurt, kulingana na msemaji wa serikali ya Berlin.

https://p.dw.com/p/4kKnr
Scholz na Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipokutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mwaka janaPicha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa  kukutana hii leo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Frankfurt, kulingana na msemaji wa serikali ya Berlin. Mazungumzo ya ana kwa ana ya viongoz hao, yatafanyika wakati washirika wa kijeshi wa Ukraine ikiwemo Marekani, wakikusanyika katika kambi ya anga ya Washington iliyoko Ujerumani kuratibu uungaji mkono zaidi kwa Kyiv.

Soma: Zelensky ahudhuria mkutano Berlin

Gazeti la Ujerumani la Der Spiegel limeripoti kwamba Zelensky pia atahudhuria mkutano huo katika kituo cha anga cha Ramstein, kusini magharibi mwa Frankfurt. Zelensky atajaribu kuwarai washirika wake msaada zaidi kwa mujibu wa gazeti hilo, ikiwa ni siku chache baada ya watu 55 kuuawa na 300 kujeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi kwenye mji wa Poltava. Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin atakuwa mwenyeji wa mkutano huo.