Zelensky asaini mkataba wa usalama na Ujerumani
16 Februari 2024Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani, mkataba huo ni wa thamani ya dola bilioni 1.22 na unalenga kuimarisha ulinzi wa anga na kuongeza silaha za kivita.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, alisema makubaliano hayo ya usalama na Ukraine ni ya kihistoria na kwamba kwa mara ya kwanza "serikali ya Ujerumani inasimama kama nchi mdhamini."
Zelensky pia alitarajiwa kusaini makubaliano kama hayo na Ufaransa jioni ya Jumatano (Februari 16), wakati akisaka msaada wa ziada kwa vikosi vyake vinavyokabiliwa na mashambulizi makali ya Urusi katika uwanja wa mapigano mashariki mwa Ukraine kwa sababu ya uhaba wa silaha.