1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky asema atapinga mipango yote isiyoihusisha Ukraine

18 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekosoa mipango yoyote ya kufikia makubaliano na Urusi bila ya kuihusisha nchi yake baada ya Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4iTVG
Ukraine | Vita | Rais Volodymyr Zelensky akiwa Kyiv
Rais Volodymyr Zelensky akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kyiv, Julai 15, 2024Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Akiwahutubia viongozi wa Ulaya katika mkutano wa kilele unaofanyika katika kasri la Blenheim nchini Uingereza, Zelensky ametoa wito wa kuwepo "umoja” na kuiunga mkono nchi yake katika vita vyake na Urusi.

Wito wa Ulaya wa kuzungumza kwa kauli moja umetolewa baada ya Orban, kumtembelea Putin mjini Moscow katika ziara iliyokosolewa vikali na viongozi wa Ulaya.

Waziri Mkuu huyo wa Hungary alifanya ziara aliyoiita "Ujumbe wa Amani" mjini Moscow mnamo Julai 5.