1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky atoa mwito wa kupatiwa silaha zenye nguvu zaidi

Sylvia Mwehozi
9 Septemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya jana kwamba hatua za mataifa ya magharibi za kuisambazia silaha nchi yake zinakwenda taratibu mno na hivyo kudhoofisha juhudi zake za kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4W8ZZ
Ukraine Kiew | Videoansprache von Wolodymyr Selenskyj
Picha: president.gov.ua

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonya jana kwamba hatua za mataifa ya magharibi za kuisambazia silaha nchi yake zinakwenda taratibu mno na hivyo kudhoofisha juhudi zake za kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

Kwenye taarifa yake iliyochapishwa katika tovuti ya serikali, Zelensky amedai kuwa michakato yote imezidi kuwa migumu na ya kusuasua, akimaanisha vikwazo na usambazaji wa silaha. Kiongozi huyo ameendelea kuyashawishi mataifa ya magharibi kuipatia Kyiv silaha zenye nguvu zaidi na za masafa marefu ili iweze kuvifurusha vikosi vya Urusi.Zelensky alaani shambulizi la Urusi lililowaua watu 16

Matamshi yake yanakuja wakati Urusi ikifanya uchaguzi wa serikali za mitaa katika maeneo iliyoyanyukua, uchaguzi ambao umekosolewa na Ukraine na makundi ya kimataifa. Urusi ilitangaza kwamba mikoa ya Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia, Kherson pamoja na Crimea itafanya uchaguzi.