Zelensky atoa wito wa ushirikiano dhidi ya vita vya Urusi
29 Desemba 2023Katika hotuba yake aliyotoa siku ya Alhamisi jioni kupitia njia ya video kabla ya mwisho wa mwaka, Zelensky amesema kuwa ''ugaidi'' wa Urusi lazima ushindwe na kuongeza kuwa wote walioko katika ulimwengu huru lazima wahakikishe hilo kwa pamoja.
Soma pia: Urusi yaionya Japan dhidi ya kuipa Ukraine mfumo wa ulinzi wa anga
Zelensky pia alimshkuru kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis kwa risala za kheri njema na amani kwa Ukraine na Marekani kwa msaada wake wa kijeshi wa hivi karibuni wa makombora mapya ya ulinzi wa anga.
Awali, Zelensky alimteua gavana mpya wa mkoa wa Donetsk ulioko Mashariki mwa nchi hiyo, ambao unapiganiwa na vikosi vya Ukraine na Urusi.
Soma pia: Marekani imetangaza msaada wa mwisho wa silaha kwa Ukraine
Zelensky, alimteua Vadym Filashkin kupitia amri ya rais iliyochapishwa jana Alhamisi.
Filashkin amekuwa naibu gavana wa eneo hilo tangu Februari mwaka 2019.