1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky awashawishi Wamarekani kuendelea kuisaidia Ukraine

13 Desemba 2023

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema nchi yake imefanikiwa katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi, ingawa amesisitiza umuhimu wa umoja dhidi ya uchokozi wa Kremlin.

https://p.dw.com/p/4a5nw
Rais Volodymyr Zelensky (kulia) na mwenyeji wake, Rais Joe Biden wa Marekani.
Rais Volodymyr Zelensky (kulia) na mwenyeji wake, Rais Joe Biden wa Marekani.Picha: CHIP SOMODEVILLA/AFP/Getty Images

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake, Rais Joe Bidenwa Marekani, katika Ikulu ya White House hapo jana, Zelensky amesema ziara yake ya sasa ya Washington ina lengo la kuyaelezea yaliyo muhimu, hasa jinsi ya kuishinda Urusi kwenye vita vya angani.

Soma zaidi: Zelensky anatarajiwa kukutana na Biden mjini Washington

Awali, Zelensky alikuwa na mazungumzo ya faragha na maseneta na mwenyekiti wa wajumbe wa Republican katika Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson.

Soma zaidi: Zelensky ameonya dhidi ya kusambaratika kwa ushirikiano wa mataifa ya Magharibi

Msaada mpya wa Marekani kwa sasa umezuiwa na bunge kutokana na mzozo kati ya Republican na chama cha Democrat, chake Rais Biden. Johnson alisema msimamo wa chama chake wa kutilia shaka msaada kwa Ukraine bado haujabadilika.