Zelensky kukutana na viongozi wa Ujerumani na Ufaransa
16 Februari 2024Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuwasili mjini Berlin na Paris hii leo na kukutana na viongozi wa mataifa hayo mawili. Akiwa mjini Berlin, Zelensky atakutana na kutia saini mikataba ya ushiriikiano wa kiusalama na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani. Kisha baadae ataelekea mjini Paris kwa ajili ya kutia saini mikataba kama hiyo na Rais Emmanuel Macron.
soma:Biden and Scholz kujadiliana juu ya msaada mpya kwa Ukraine
Zelenskyy pia anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa usalama wa Munich unaoanza mwishoni mwa juma hili, ambao utahudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali wapatao 40 pamoja na wataalam wengi wa kijeshi.
Ziara ya Zelensky katika mataifa hayo makubwa ndani ya Umoja wa Ulaya, inafanyika wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukiingia mwaka wa tatu huku vikosi vyake vikikabiliwa na hali ngumu upande wa mashariki.