1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Nitaunga mkono India kuandaa mkutano wa amani

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mazungumzo yanaendelea na Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Uswisi kuhusiana na mkutano wa pili unaolenga usitishwaji wa kudumu wa mapigano Ukraine.

https://p.dw.com/p/4jtpb
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Juan Carlos Rojas/picture alliance

Zelenskiy amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari wa India na kuongeza kwamba amemwambia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwamba angeliunga mkono India kuwa mwandaaji wa mkutano wa pili wa amani.

Aidha Zelensky aliongeza kwamba hawataweza kufanya mkutano wa kilele wa amani katika nchi ambayo bado haijajiunga kwenye tamko la mkutano wa kilele wa amani kuhusu Ukraine. 

Soma pia:Modi amrai Zelensky kukaa mezani kumaliza vita na Urusi

Wakati hayo yakiendelea mwandishi wa habari wa shirika la Reuters hajulikani alipo na wengine wawili wamejeruhia kufuatia shambulio la Urusi kwenye moja ya hotel katika mji wa Kramatorsk nchini Ukraine.

Moscow imeendelea na mkururo wa mashambulizi yake na kusonga mbele mashariki mwa Ukraine licha ya mashambulizi makubwa ya Ukraine katika eneo la Kursk nchini Urusi.