1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe: Ni wakulima wa kigeni tu watakaorejeshewa ardhi

2 Septemba 2020

Serikali ya Zimbabwe imesema ni wakulima wa kigeni tu ambao walikuwa wakilindwa na mkataba wa kimataifa wanaokidhi vigezo vya kurejeshewa ardhi yao ambayo ilitaifishwa na serikali miongo miwili iliyopita.

https://p.dw.com/p/3htql
Simbabwe Landreform Weiße Farmer
Picha: Getty Images/D. Kitwood

Mwaka 2000 Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe alianzisha mabadiliko ya sera ya ardhi, na kutwaa ardhi hiyo kutoka kwa wakulimia takribani 4,000  wa kizungu, kwa kile alichodai kurejesha umiliki wa asili, na kuondosha hali iliyokuwepo ya kutoa upendeleo kwa jamii ya wazungu wachache. Hapo Jumatatu, serikali ilisema wakulima wazungu wanaweza kuomba ridhaa ya kurejeshewa hati za umiliki wa ardhi yao. Lakini Jumannne, Katibu wa wizara ya habari na msemaji wa serikali, Nick Mangwana alifafanua katika ukurasa wake wa twitter kwamba fursa hiyo haitowahusu wakulima wote wazungu waliofukuzwa, isipokuwa kwa wakulima 37 wa kigeni wanaofaidika na kinga maalum ya kisheria.