SiasaAfghanistan
Afghanistan yahimiza mazungumzo na jamii ya kimataifa
30 Januari 2024Matangazo
Amir Khan Muttaqi aliyasema hayo katika mkutano mjini Kabul uliowaleta pamoja wajumbe maalum na wawakilishi kutoka nchi 11, zikiwemo China, Urusi, Iran, Pakistan na India.
Ametoa wito wakukuza ushirikiano wa kikakanda kwa ajili ya ushirikiano wenye tija ili kupambana na vitisho vilivyopo na vinavyoweza kujitokeza katika kanda hiyo.
Soma pia:Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kuteuliwa kwa mjumbe maalum kwa Afghanistan
Serikali ya Taliban mjini Kabul haijatambuliwa rasmi na serikali yoyote nyingine tangu ilipochukua madaraka mwaka wa 2021, na kuweka tafsiri kali ya sheria za Kiislamu ambazo zimewawekea vikwazo wanawake kushiriki katika karibu kila sekta ya maisha ya umma.