Matukio na masuala ya barani Afrika yaliyozingatiwa na magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii ni pamoja na madhara yaliyolikumba jimbo la nje la Ufaransa la Mayotte, kutokana na kimbunga Chido. Mazungumzo juu ya kuleta amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yavunjika na juu ya mwisho wa mshikamano kati ya wakomunisti na chama cha ANC nchini Afrika Kusini. Mtayarishaji Zainab Aziz