1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yazuia kusarifishwa watoto 400 wa Zimbabwe

4 Desemba 2023

Maafisa wa mpakani nchini Afrika Kusini wameyazuia mabasi kadhaa yaliyokuwa yamewabeba watoto zaidi ya 400 kutoka Zimbabwe.

https://p.dw.com/p/4ZlGX
Watoto barani Afrika.
Watoto barani Afrika.Picha: JOHN WESSELS/AFP

Kamishna wa Shirika la Kusimamia Mipaka la Afrika Kusini, Mike Masiapato, amesema waliyasimamisha na kuyapekuwa mabasi 42 usiku wa kuamkia Jumapili (Disemba 3) na kuwapata watoto 443 walio chini ya umri wa miaka 8.

Taarifa zinasema kuwa watoto hao hawakuwa wameambatana na wazazi ama walezi na hivyo walizuiliwa katika operesheni ya kupambana na usafirishaji haramu wa binaadamu.

Soma zaidi: UNICEF: Watoto milioni 13 Afrika hawakupewa chanjo
Wanawake Zimbabwe wapambana dhidi ya ubaguzi wa kijinsia

Kwa mujibu wa maafisa wa Afrika Kusini, watoto hao walikuwa wakisafirishwa kinyemela kuingia nchini humo.

Hata hivyo, shirika linalowawakilisha raia wa kigeni waishio Afrika Kusini limesema kuna uwezekano watoto hao walikuwa wakisafirishwa kuwaona wazazi wao wanaofanya kazi nchini humo.

Zaidi ya Wazimbabwe milioni moja wanaishi Afrika Kusini, wengi wao kinyume cha sheria, na ambao wamehamia miaka 15 iliyopita.