Wakuu wa ECOWAS kukutana wikendi hii kutathmini mahusiano
6 Julai 2024Nchi za Afrika Magharibi zilizogawanyika zinaandaa mikutano miwili ya marais wikiendi hii. Mmoja unafanyika leo mjini Niamey nchini Niger kati ya viongozi wa utawala wa kijeshi wa eneo la Sahel, ukifuatiwa na mwingine nchini Nigeria hapo kesho ukiwahusisha viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.
Wakuu wa Mali, Burkina Faso na Niger ambazo zilijitoa kwenye jumuiya hiyo ya kiuchumi Januari wmaka huu wanakatutana kwa mara ya kwanza tangu waingie madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi kati ya 2020 na 2023. Mkutano huo wa leo ni wa kwanza kati ya viongozi wa muungano mpya wa nchi za eneo la Sahel, Alliance of Sahel States, AES, na unatarajiwa kupitisha maazimio.
Soma zaidi.Masoud Pezeshkian ashinda uchaguzi wa rais Iran
Mkutano wa kilele wa hapo kesho utafanyika mjini Abuja nchini Nigeria na utatoa fursa wakuu wa jumuiya ya ECOWAS kujadilia mahusiano na muungano wa nchi za Sahel. Mkutano huo unakuja wakati marais kadhaa wa Afrika Magharibi wakitoa mwito wa kutafuta suluhu ya kuanza tena mazungumzo kati ya kambi hizo mbili, hasa, Rais mpya wa SenegalBassirou Diomaye Faye aliyesema kwamba maridhiano kati ya ECOWAS na nchi hizo tatu za Sahel yanawezekana.