Al-Sharaa: Raia wa Syria wanapaswa kujiamulia wenyewe
23 Desemba 2024Kiongozi huyo wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham HTS baada ya kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema ni muhimu kwa wahusika wakuu wakubaliane juu ya masuala muhimu kuhusu nchi hiyo.
al-Sharaa anayejulikana pia kama Abu Mohammed al-Joulani ameeleza kuwa raia wa Syria wanapaswa kupewa nafasi ya kujiamulia wenyewe juu ya usalama wa nchi yao hasa baada ya mateso yaliyopitia katika utawala uliopita.
Soma pia: Kiongozi mpya Syria aahidi kuheshimu mamlaka ya Lebanon
Kundi la Hayat Tahrir al-Sham liliunda serikali ya mpito nchini Syria baada ya kuongoza mashambulizi ya waasi yaliyomng'oa madarakani Bashar al-Assad mapema mwezi huu.
Uturuki inachukuliwa kuwa moja ya nchi zenye ushawishi mkubwa ndani ya Syria, japo Urusi, Iran na Marekani pia zimeonekana kwa kiasi fulani kuwa na ushawishi ndani ya nchi hiyo.