Al-Shibani aiambia Iran isieneze machafuko nchini Syria
25 Desemba 2024Al-Shibani ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa X kuwa, Iran ni lazima iheshimu matakwa ya Wasyria na usalama wa nchi hiyo na kwamba watawala wapya wa Damascus watawawajibisha kutokana na kauli zao.
Hata hivyo waziri huyo mpya wa mambo ya nje wa Syria hakuweza wazi alikuwa akimlenga nani.
Soma pia: Kiongozi mpya Syria aahidi kuheshimu mamlaka ya Lebanon
Kauli hiyo ya Al-Shibani imejiri baada ya kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei kuwahimiza vijana wa Syria kusimama kwa ujasiri dhidi ya watu waliopanga na kusababisha ukosefu wa usalama nchini humo.
Kuondolewa madarakani kwa Bashar al-Assad kunachukuliwa kama pigo kwa muungano wa kisiasa na kijeshi unaoongozwa na Iran unaofahamika kama "mhimili wa upinzani” unaopinga ushawishi wa Israel na Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.