1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Idadi ya watu walionyongwa duniani yaongezeka mno

16 Mei 2023

Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema katika ripoti yake kuwa idadi ya watu waliouawa kwa kunyongwa ulimwenguni kote mwaka uliopita, imeongezeka kwa asilimia 53.

https://p.dw.com/p/4RSAG
Symbolbild | Galgen und Schlinge
Picha: Allison Bailey/NurPhoto/picture alliance

Amnesty imesema idadi hiyo imefikia watu 883. Hiyo ni idadi ya juu zaidi ya matukio hayo tangu mwaka 2017. 

Ripoti ya shirika hilo imeyashutumu hasa mataifa ya mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika, ikiwa ni pamoja na Iran, Saudi Arabia na Misri, ambayo yanafahamika kwa kutekeleza adhabu ya kifo.

Amnesty: Idadi ya watu walionyongwa iliongezeka mwaka 2022

Ripoti hiyo imebaini kuwa usiri wa serikali za Korea Kaskazini na Vietnam pamoja na upatikanaji duni wa taarifa katika nchi kadhaa, vinazuia utoaji wa tathmini kamili ya hukumu ya vifo.

Amnesty imesema matendo hayo yanakiuka sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.