Ankara. Bunge la Uturuki lachagua rais mpya.
27 Aprili 2007Wakati kura zikiendelea kupigwa bungeni katika hatua ya kumchagua rais mpya wa Uturuki , chama tawala chenye kuelemea upande wa kidini kinaweza kupambana na ususiaji wa uchaguzi.
Chaguo la chama cha haki na maendeleo la waziri wa mambo ya kigeni Abdullah Gul kuwa kama mgombea wao kimeanza kuleta hali ya wasi wasi.
Chama kikuu cha upinzani cha Republican Peoples Party kimetishia kususia uchaguzi huo , kwasababu hakushauriwa kuhusu Gul.
Gul alianza shuguli za siasa katika chama kilichopigwa marufuku cha Kiislamu, hata hivyo amekuja kujulikana kuwa ni mfuasi wa siasa za wastani. Iwapo hatafikisha kiasi kinachotakiwa cha wingi wa theluthi mbili katika duru ya kwanza , upigaji kura utaingia katika duru ya pili itakayofanyika katika mwezi wa Mei.