1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Bunge la uturuki laidhinisha mageuzi.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3D

Bunge la Uturuki limeidhinisha mageuzi makubwa ya katiba ambayo yatasababisha rais wa baadaye wa nchi hiyo kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi badala ya bunge.

Mabadiliko hayo yanapaswa bado kutiwa saini na rais Ahmet Necdet Sezer.

Chama tawala chenye ngome yake katika Uislamu cha Haki na maendeleo AKP kimesukuma mageuzi hayo kupita katika bunge baada ya upande wa upinzani unaotaka utengano wa dini na serikali kupinga juhudi mara mbili za serikali za kumpitisha waziri wa mambo ya kigeni Abdullah Gul kuchaguliwa kuwa rais.

Uchaguzi huo wa rais umeahirishwa hadi pale uchaguzi mkuu wa Uturuki utakapofanyika mwezi Julai.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanatarajia kuwa rais wa sasa Sezer , ambaye anapendelea mtengano wa dini na serikali , atarejesha muswada huo wa mageuzi bungeni.