ANKARA: Bunge la Uturuki launga mkono mageuzi ya kikatiba
11 Mei 2007Matangazo
Bunge la Uturuki limeidhinisha mswada wa kufanywa marekebisho makubwa ya katiba.Mswada huo unapendekeza kuwa katika siku zijazo rais achaguliwe na wapiga kura badala ya kuchagiliwa na wabunge.Hata hivyo marekebisho hayo yanahitaji kutiwa saini na Rais Ahmed Necdet Sezer.Chama tawala cha AKP kimepitisha mswada huo bungeni, baada ya chama cha upinzani kupinga mara mbili juhudi za serikali za kutaka kumchagua waziri wa mambo ya kigeni Abdullah Gul kama rais mpya. Sasa uchaguzi wa rais umeahirishwa na utafanywa baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Julai.