1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Gül atarajia kuchaguliwa rais

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBV7

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki, Abdullah Gül, anatajia kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Uturuki hii leo.

Bunge la Uturuki linapiga kura kwa mara ya tatu leo mchana ambapo chama tawala cha AK kinahitaji wingi wowote wa kura kushinda nafasi hiyo.

Chama cha AK kina idadi ya viti 341 kati ya viti 550 bungeni, hivyo bwana Gül anatarajwia kuwashinda wagombea wengine wawili wanaowania pia wadhifa huo wa rais.

Kamanda wa jeshi la Uturuki, Yasar Buyukanit, amesema anaona kuna njama ya kutaka kuihujumu Uturuki, matamshi yanayopendekeza kwamba jeshi hilo halitakaa kimya litakapoona maswala ya dini na taifa yakiunganishwa.

Masoko ya fedha nchini Uturuki yameathirika kufuatia matamshi ya kamanda huyo wa jeshi huku lira moja ya Uturuki ikiuzwa kwa kiwango cha 1.32 dhidi ya dola ya Marekani.