ANKARA: Rais wa Israel kuhotubia Bunge la Uturuki
12 Novemba 2007Matangazo
Rais wa Israel Shimon Peres amewasili mji mkuu wa Uturuki,Ankara kwa ziara ya kihistoria.Siku ya Jumanne,Peres atakuwa rais wa kwanza wa Kiisraeli kuhotubia bunge la nchi hiyo ya Kiislamu.
Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas pia anatazamiwa Ankara na atawahotubia wabunge wa Uturuki baadae siku hiyo hiyo.Peres amesema,Uturuki huenda ikaweza kutoa mchango muhimu katika mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati.