ANKARA:Mkewe Rais Gul anyimwa mualiko na jeshi la Uturuki
31 Agosti 2007Rais mpya wa Uturuki Abdula Gul anahudhuria sherehe za kijeshi za siku ya Ushindi huku mkewe akibezwa na jeshi kwa kutoalikwa.Bwana Gul aliyeteuliwa siku ya Jumanne alikaa katikati ya Waziri Mkuu Recep Tayip Erdogan na mkuu wa majeshi Yasar Buyukanit bila kusemezana.
Mkewe rais Bi Hayrunnisa Gul anayejifunga mtandio kwa kawaida anatazamwa kama nembo ya siasa zilizo na misingi ya uislamu hakuhudhuria sherehe hizo aidha mkewe Waziri Mkuu Erdogan ambaye pia hujifunga hijabu.
Tangu kuteuliwa kwake jeshi la taifa linakataa kumuonyesha kiongozi wake mpya heshima jambo linalokosolewa hata na wanaompinga Rais Gul.jeshi kwa kawaida hukataa kuwaalika wake za maafisa wa serikali wanaovaa mitandio ila hii ni mara ya kwanza kwa mkewe rais kudharauliwa.Jeshi hilo aidha linahakikisha kuwa sheria iliyowekwa ya kupinga marufuku uvaaji wa hijabu katika afisi za serikali na vyuo vikuu inatimizwa.
Wake wa maafisa wa kijeshi ambao hujifunga mtandio hawapandishwi cheo na kufukzwa jeshini.
Uteuzi wa Bwana Gul ni ushindi mkubwa wa chama cha AKP dhidi ya wafuasi wa uongozi usio na misingi ya kidini waliopinga uteuzi wake wa kwanza mwezi Aprili.