You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
13.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Taarifa ya Habari ya Asubuhi ya leo ina mengi lakini makubwa ni: Rais mteule wa Marekani Donald Trump aendelea kufanya teuzi, akiunda serikali yake mpya: Marekani yazizuia ndege za kiraia kwenda Haiti baada ya ndege moja kushambuliwa ilipokuwa inaingia Haiti: Na Somaliland yafanya uchaguzi wa rais katikati ya mzozo wa kidiplomasia. Sikiliza zaidi.
12.11.2024 Matangazo ya Jioni
Israel inaendeleza mashambulizi huko Gaza na nchini Lebanon// (Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, ametangaza wajumbe wapya wa serikali yake inayokuja//Wadau wa elimu barani Afrika wamejumuika jijini Dar es Salaam leo kujadili changamoto na fursa mbalimbali za kuimarisha mifumo ya elimu.
12.11.2024 Matangazo ya Mchana
Takriban mataifa 200 yamekusanyika katika mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi, COP29// Viongozi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu waliokutana jana nchini Saudi Arabia, wametoa wito wa usitishwaji vita huko Gaza na nchini Lebanon huku wakisisitiza kwamba kuondoka kwa Israel katika maeneo ya Palestina.
Tunatafuta Neno la Mwaka 2024
Shiriki katika kura ili kusaidia kuamua Neno la Mwaka 2024 na upate bahati ya kushinda seti ya DW
12.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Warepublican, ambao wana mipango mikubwa, huenda wataongoza Ikulu ya White House na mabunge yote mawili ya Congress//Umoja wa Mataifa umesema ushawishi wa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika sehemu za mashariki mwa Kongo sasa umeongezeka//Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unafunguliwa rasmi hii leo mjini Baku, Azerbaijan.
11.11.2024 Matangazo ya Jioni
Mkutano wa kilele wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, unaendelea Baku nchini Azerbaijan// Jeshi la Polisi Zanzibar linasema linafanya uchunguzi wa vifo vya watu wawili vilivyotokea kaskazini mwa kisiwa cha Unguja vinavyohusishwa na vikosi vya usalama.
11.11.2024 Matangazo ya Mchana
Urusi na Ukraine zimeshambuliana usiku wa kuamkia leo// Mkutano wa kilele wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, umeanza leo mjini Baku nchini Azerbaijan// Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema yuko tayari kuitisha kura ya imani juu yake katika mwaka huu wa 2024 iwapo pande zote zitaridhia ili kuwezesha kuitishwa uchaguzi wa mapema.
11.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
11.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza Taarifa ya Habari ya Asubuhi, ambapo miongoni mwa mengineyo utasikia Rais mteule wa Marekani Donald Trump afanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi: Haiti yamteua Waziri Mkuu mpya, hatua inayotishia mzozo zaidi kwenye taifa hilo la kisiwa: Na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aashiria utayari wa kuitisha mapema kura ya imani ya bunge.
Matangazo ya Jioni 10.11.2024
Dunia yetu leo Jioni 10.11.2024
Droni 62 kati ya 45 za Urusi zadunguliwa Ukraine
Jeshi la anga la Ukraine mapema leo limesema limezidungua droni 62 kati ya 145 zilizorushwa na Urusi nchini humo.
Qatar yajiondowa upatanishi vita vya Gaza
Qatar imejiondowa kwenye upatanishi wa kusaka makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza na kuachiliwa kwa mateka.
Waasi wauwa 26 Baluchistan
Mashambulizi ya bomu yaliyofanywa na kundi linalopigania kujitenga nchini Pakistan yameuwa watu 26.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Amina Abubakar ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki hii, ikiwemo kile kinachoendelea Marekani, Donald J Trump kurejea tena madarani kama rais wa 47 wa taifa hilo. Je ushindi wake una maana gani kwa Bara la Afrika? Nchini Msumbiji ghasia za baada ya uchaguzi zashuhudiwa na Kongo na Rwanda zathibitisha haja ya kuheshimu usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo.
Viongozi wa Ulaya waahidi mageuzi ya kiuchumi
Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana Budapest, Hungary wameahidi kuufanyia mageuzi ya haraka uchumi wa kanda hiyo.
08.11.2024 Matangazo ya Jioni
Viongozi wa Ulaya wameungana na Israel na Uholanzi kulaani vurugu zilizoibuka baada ya mechi kati ya timu za Maccabi Tel Aviv na Ajax ya Amsterdam+++Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema watu wapatao 30 wameuawa nchini Msumbiji.
08.11.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Israel alaani mashambulizi mjini Amsterdam/ Viongozi wa EU wajadili mikakati ya kujiimarisha
Raia ni 70% ya waliouawa Gaza - Umoja wa Mataifa
Umoja wa Mataifa unasema takribani 70% ya waliouawa kwenye vita vya Gaza ni wanawake na watoto.
Msikiti wa miaka zaidi ya 450 wa Mombasa Kenya
Msikiti wa kipekee duniani kwa kuwa na sehemu mbili ambazo Waislamu hutazama kuelekea Makka wanaposwali.
07.11.2024 Matangazo ya Jioni
Ujerumani imejikuta leo katika mtikisiko wa kisiasa baada ya Kansela Olaf Scholz kumfuta kazi Waziri wake wa fedha//Polisi nchini Msumbiji leo wametumia mabomu ya kutoa machozi pamoja na mbwa kuwatawanya waandamanaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi//Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuhutubia taifa leo Alhamisi baada ya chama chake cha Democratic kushindwa katika uchaguzi.
07.11.2024 Matangazo ya Mchana
Naibu Kansela Robert Habeck amesema leo kuwa serikali bado inaweza kuendelea kufanya kazi hata baada ya Kansela Olaf Scholz kumfuta kazi waziri wake wa fedha Christian Lindner// Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekubali mwaliko wa rais anayeondoka madarakani Joe Biden katika Ikulu ya White House// Maandamano ya kupinga matokeo ya uchuguzi yanaenedelea Msumbiji.
06.11.2024 Matangazo ya Jioni
Mgombea wa Republican, Donald Trump, anajiandaa kuanza muhula wa pili wa kihistoria madarakani kama rais wa 47 wa Marekani/ Salamu za pongezi kutoka kwa viongozi wa dunia zimeendelea kumiminika kwa Trump
06.11.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Donald Trump yupo kwenye hatihati ya kutwaa ushindi wa urais leo hii Jumatano baada ya kushinda jimbo la Pennsylvania/ Viongozi wa dunia wamimina pongezi kwa Trump
06.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais inaendelea nchini Marekani, baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa mida ya jioni kwa saa za Marekani.
05.11.2024 Matangazo ya Jioni
Wapiga kura nchini Marekani wanapiga kura katika uchaguzi huu wa rais wenye ushindani mkali na usiotabirika kuamua nani kati ya Kamala Harris na Donald Trump watakaempeka ikulu ya White House ifikapo Januari 20. Harris, makamu wa rais wa sasa wa chama cha Democratic, na Trump, rais wa zamani anaepeperusha bendera ya Republican kwa mara ya tatu mfululizo
Zelensky adai wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wako Kursk
Zelensky amedai wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wamewasili katika mpaka wa nchi yake na Urusi kwenye eneo la Kursk.
Wamarekani wafanya uchaguzi wa kihistoria
matokeo ambayo yanatarajiwa kusababisha mshutuko na hisia mseto kote ulimwenguni.
05.11.2024 Matangazo ya Mchana
Harris ama Trump? Wapiga wa Marekani wanaamua leo Jumanne// Ufuatiliaji wa Afrika katika uchaguzi wa Marekani ni mkubwa huku kukiwa na mitazamo tofauti // Mashambulizi ya Israel yamewaua Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza
Watu 30 wauawa katika mashambulizi ya Israel Gaza
Mashambulizi ya Israel yamewaua Wapalestina wasiopungua 30 kwenye Ukanda wa Gaza.
04.11.2024 Matangazo ya Jioni
Mashambulizi ya makombora ya Israel yamesababisha vifo vya huko Gaza// Makamu wa rais Kamala Haris wa chama cha Democratic na rais wa zamani wa chama cha Republican Donald Trump wanaendelea kunadi sera zao// Wataalamu mbalimbali barani afrika wanakutana nchini Tanzania kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wadogo.
04.11.2024 Matangazo ya Mchana
Kampeni za urais nchini Marekani zimeingia dakika za lala salama kuelekea uchaguzi mkuu wa kesho// Israel imesema leo kuwa imesitisha mahusiano yake na Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi wa Palestina UNRWA// Maafisa wa afya wasema hakuna ongezeko la maambukizi ya virusi vya mpox katika katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
03.11.2024 Matangazo ya Jioni
Jeshi la Israel latoa agizo kwa wakaazi wa Baalbek nchini Lebanon kuhama+++ Harris apiga kampeni Michigani, Trump yupo majimbo ya maamuzi ya Mashariki+++Radi yaua watu 14 katika Kanisa kwenye kambi ya waikimbizi Uganda
03.11.2024 Matangazo ya Mchana
Kiongozi wa Juu wa Iran aapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel+++Chama cha BSW chashinikiza msimamo wake dhidi ya silaha kwa Ukraine+++Machafuko yaendelea kushuhudiwa Msumbiji
Matangazo ya Jioni: 02.11.2024
Shambulizi la Israel laua watu 42 ndani ya saa 24 huko Gaza. Mtu mmoja ameuawa na wengine 46 wamejeruhiwa kwenye mashambuli ya Urusi nchini Ukraine. Waziri Mkuu wa Hungary, Victor Orban anataka Trump ashinde urais wa Marekani. Kiongozi wa Guinea ajipandisha cheo na kuwa Jenerali wa jeshi.
01.11.2024-Matangazo ya Jioni
Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati ameitupia lawama Israel kwa kukataa usitishaji vita ikiwa ni baada ya jeshi la Israel kushambulia ngome ya Hezbollah+++Wanasiasa nchini Tanzania hii leo wamehitimisha shughuli ya kurejesha fomu kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaaa unaofanyika baadaye mwezi huu.
01.11.2024 - Matangazo ya Mchana
Hatimaye, Kenya inafungua ukurasa mpya kisiasa baada ya kupata naibu mpya wa rais ambaye ni Profesa Kithure Kindiki aliyekuwa waziri wa usalama wa taifa.Kindiki ameapishwa rasmi asubuhi hii kuwa naibu wa rais wa tatu+++Chama tawala cha Botswana BDP kimeshindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 30. Ushindi huo unahitimisha miaka 58 ya utawala wa chama hicho madarakani.
31.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Mahakama Kuu nchini Kenya imefutilia mbali amri iliyomzuwia waziri wa usalama wa taifa Kithure Kindiki kuapishwa rasmi kuwa naibu wa rais mpya. Hilo ni pigo jipya kwa kambi ya Rigathi Gachagua aliyetimuliwa katikati ya mwezi huu wa Oktoba+++Vikosi vya Urusi vimeshambulia jengo la makazi katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine leo, na kuwaua watu watatu
31.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Maafisa wa Palestina wamesema jeshi la Israel liliuvamia Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu ambapo watu watatu wameuawa+++Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, hapo jana alifanya alifanya ziara ya masaa kadhaa mjini Entebbe, Uganda na kukutana na Rais Yoweri Museveni.
30.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Kamala Harris, amewataka wafuasi wake kukataa machafuko na mgawanyiko anaouhusisha na mpinzani wake Donald Trump+++Makundi ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya yametoa wito kwa serikali kutangaza mauaji ya wanawake na wasichana nchini humo kama janga la kitaifa baada ya visa vya mauaji kuongezeka.
30.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Jeshi la Israel linadai kuwa limeyashambulia zaidi ya maeneo 100 ya kundi la Hizbullah ndani ya Lebanon ndani ya masaa 24+++Ripoti ya tume iliyoundwa na Papa Francis kwa ajili ya ulinzi wa watoto iliyotolewa Jumanne, imesema kuwa Kanisa Katoliki linapaswa kurahisisha mchakato wa kuwaondoa mapadri waliowanyanyasa kingono watoto
30.10.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Muungano wa serikali wa Ujerumani unakabiliwa na mvutano mkubwa huku mizozo ya ndani ikiongezeka kabla ya uchaguzi wa 2025+++Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema watu wasiopunguwa 11 waliuwawa na zaidi ya 50 walijeruhiwa kwenye vurugu zilizozuka baada ya uchaguzi ulioibuwa mvutano nchini Msumbiji
30.10.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Kamala Harris ahimiza umoja wakati akiahidi kuwa rais wa Wamarekani wote // Ukraine yatangaza usajili mpya wa wanajeshi wakati Urusi ikiendelea kusonga mbele mashariki mwa nchi hiyo // Na Botswana yapiga kura huku chama tawala kikilenga kurefusha utawala wake wa miongo sit
29.10.2024 Matangazo ya Jioni
Shambulio la Israel lauwa Wapalestina kiasi 34 Kaskazini mwa Gaza+++Ujerumani imemrejesha balozi wake nchini Iran na kumwita mjumbe wa Iran kuwasilisha malalamiko kuhusu kunyongwa kwa raia wa Ujerumani na Iran, Jamshid Sharmahd+++Orban: Uchaguzi wa Georgia ulikuwa huru+++Wito wa kuunga mkono ajenda ya matumizi ya nishati safi watolewa kwa wake wa Marais Afrika
29.10.2024 Matangazo ya Mchana
Shambulio la Israel lauwa Wapalestina kiasi 34 Kaskazini mwa Gaza+++Marekani yasema Korea Kaskazini umetuma wanajeshi 10,000 Urusi+++Mahakama ya Kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasikikiza kesi mbili zinazohusika na majaribio ya kuupinduwa utawala wa Rais Félix Tshisekedi+++Vuguvugu kubwa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaaa nchini Tanzania.
29.10.2024 Matangazo ya Asubuhi
Viongozi wa Jordan, Misri, na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, wamekosoa vitendo vya Israel katika Ukanda wa Gaza na Lebanon+++Hakuna shaka kwamba uchaguzi wa Marekani ndio utakaobainisha mwenendo wa vita nchini Ukraine+++Kundi la mamluki wa kirusi la Wagner, limekuwa likifanya kazi katika nchi nyingi za Afrika kwa miaka mingi.
29.10.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Israel yapiga marufuku operesheni za shirika la wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA // Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini aelekea Urusi wakati sakata la vikosi vya Pyongyang nchini Urusi likiendelea // Na Rodri ashinda tuzo ya Ballon d'Or
28.10.2024- Matangazo ya Jioni
Katibu mkuu wa Jumuiya ya NATO athibitisha wanajeshi wa Korea Kaskazini wako Urusi++Vifaru ya kijeshi vya Israel vimezidi kusogea kwenye miji kadhaa ya Kaskazini mwa Gaza++Lebanon yasema imefikisha malalamiko mbele ya baraza la usalama kuhusu shambulio la Israel lililouwa waandishi 3 wa habari
28.10.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Misri yapendekeza kusitishwa mapigano kwa siku mbili Gaza/ Georgia yajiandaa kwa maandamano baada ya kura
28.10.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa
28.10.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Iran yaapa kuchukua hatua baada ya Israel kuishambulia mifumo yake ya ulinzi // Trump amshambulia Kamala Harris katika mkutano wa kampeni New York // Na Zaidi ya watu 120 wauawa katika machafuko nchini Sudan
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 128
Ukurasa unaofuatia