You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
28.10.2024- Matangazo ya Jioni
Katibu mkuu wa Jumuiya ya NATO athibitisha wanajeshi wa Korea Kaskazini wako Urusi++Vifaru ya kijeshi vya Israel vimezidi kusogea kwenye miji kadhaa ya Kaskazini mwa Gaza++Lebanon yasema imefikisha malalamiko mbele ya baraza la usalama kuhusu shambulio la Israel lililouwa waandishi 3 wa habari
28.10.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Misri yapendekeza kusitishwa mapigano kwa siku mbili Gaza/ Georgia yajiandaa kwa maandamano baada ya kura
28.10.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa
28.10.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Iran yaapa kuchukua hatua baada ya Israel kuishambulia mifumo yake ya ulinzi // Trump amshambulia Kamala Harris katika mkutano wa kampeni New York // Na Zaidi ya watu 120 wauawa katika machafuko nchini Sudan
Matangazo ya Jioni: 26.10.2024
Jumuiya ya Madola wakubali mazungumzo kuhusu urithi wa utumwa. 50 wauawa katika mashambulizi ya wanagammbo wa RSF nchini Sudan. India na Ujerumani zakubaliana kuzalisha nishati mbadala ya hidrojeni. Georgia yafanya uchaguzi wa bunge huku mustakabali wa EU ukiwa hatarini
Matangazo ya Mchana: 26.10.2024
Israel yafanya mashambulizi ya anga ya kupiliza kisasi dhidi ya Iran. Marekani yaidhinisha mauzo ya silaha ya dola bilioni 2 kwa Taiwan yakiwemo makombora. Viongozi wa G7 wakubaliana kuhusu mkopo kwa Ukraine uliotokana na mali za Urusi. Upinzani waonya utawala wa Tshisekedi kuhusu mageuzi ya katiba
26.10.2024: Matangazo ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza Matangazo ya Asubuhi kuanzia uchambuzi wa ripoti zetu kwa kina hadi makala ambazo ni pamoja na Afrika Wiki Hii na Vijana Tugutuke. Tafadhali sikiliza hapa.
26.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa tuliyonayo kwenye taarifa a habari asubuhi hii ni pamoja na Israel yafanya mashambulizi nchini Iran: Wakuu wa kundi la G7 wakubaliana kuhusu mkopo kwa Ukraine uliotokana na mali za Urusi na Umoja wa Mataifa wasema Vita vimewaathiri zaidi ya wanawake milioni 600 pamoja na wasichana. Sikiliza kwa kina hapa.
Maoni: Sakata la Gachagua laiweka wapi Kenya?
Mahakama ya juu ya Kenya ilianza Jumanne wiki hii kusikiliza shauri la naibu wa rais Rigathi Gachagua kupinga uamuzi wa baraza la seneti kumuondoa katika nafasi yake. Ni sakata la kisiasa ambalo limeitumbukika Kenya katika mtihani na kuvuruga mwenendo wa siasa za nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni.
Jasiri anaewapambania watoto Tanzania
Glorey Nisajile, ni msichana ambaye anawasaidia watoto watokao katika mazingira magumu na kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yao ya msingi, lakini lengo lake kubwa ni kuona watoto hawa wakijilinda kutokana na ukatili ambao mara nyingi hupitia. Anatamani kuona jamii ikiwasaidia watoto hawa na si kulisahau kundi hili.
25.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Hukumu ya kifungo cha miaka 40 ambayo imetolewa kwa aliyekuwa kamanda wa kundi la waasi la LRA Thomas Kwoyelo haijawaridhisha baadhi ya waathirika wa maovu yake+++Wakenya wapinga vikali pendekezo la kuongeza muda wa Rais kubaki madarakani kutoka miaka mitano hadi saba+++Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza ameufungua mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola nchini Samoa
Umoja wa Mataifa wasema hali ya Gaza ni giza zito
Umoja wa Mataifa unasema mashambulizi ya Israel yanawazuwia raia kukimbilia maeneo salama.
Israel yauwa 28 Gaza, 3 Lebanon
Jeshi la Israel limeuwa watu 38 kwenye Ukanda wa Gaza na waandishi watatu wa habari nchini Lebanon.
25.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Mashambulizi ya anga ya Israel yameuwa watu 38 katika kitongoji cha Khan Younis kwenye Ukanda wa Gaza+++Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Ujerumani inataka kuimarisha ushirikiano wa ulinzi na India. Ameyasema hayo huku Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akitangaza fursa za kupata visa kwa raia wake wenye ujuzi wanaotaka kufanya kazi Ujerumani
25.10.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Korea ya Kusini, Jumuiya ya Kujihami ya NATO na Marekani wanadai kwamba maelfu ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wanafanya mafunzo Urusi ili kuisaidia Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine+++Kesi maarufu ya ubakaji wa jumla uliofanywa na wanaume kadhaa wakisaidiwa na mume wa mwanamke mmoja nchini Ufaransa inabainisha jinsi utamaduni wa ubakaji ulivyokita mizizi sio tu katika taifa hilo.
25.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa yaliyomo kwenye taarifa ya habari ya asubuhi ni Rais wa urusi Vladimir Putin ahitimisha mkutano wa kilele wa kundi la BRICS: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ni kinyume cha sheria: Na Bahamas yataka mazungumzo ya kweli kuhusu fidia kutokana na historia ya utumwa. Ungana nasi.
24.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Mgombea urais wa chama tawala cha Frelimo nchini Msumbiji, Daniel Chapo, ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais+++Lebanon imesema inahitaji msaada wa kimataifa ili kuimarisha jeshi lake na kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa vibaya na vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah
24.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Mji wa Kalembe, ambao ni muhimu kuelekea kwenye machimbo ya madini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulianguka tena mikononi mwa kundi la wapiganaji wa M23 tangu hapo jana mchana+++Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanadai wana ushahidi wa kutosha kwamba Korea Kaskazini imetuma wanajeshi wake nchini Urusi.
24.10.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Serikali ya Tanzania imeanzisha rasmi mchakato wa ujenzi wa Daraja la Jangwani+++Miaka miwili sasa tangu kufikiwa kwa makubaliano ya kilimwengu ya kuzuwia kusambaratika kwa mazingira asilia, kuna wasiwasi mkubwa kwamba hakuna hatua yoyote ya maana iliyopigwa
24.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa habari tulizonazo asubuhi hii ni Ujerumani na Austria zawaita mabalozi wa Korea Kaskazini kufuatia tuhuma za kuwapeleka wanajeshi wake nchini Urusi. Ufaransa yanuia kukusanya dola milioni 540 kwa ajili ya kuisaidia Lebanon na Watu watano wauawa na wengine 22 kujeruhiwa katika shambulizi kwenye kiwanda cha vifaa vya ndege nchini Uturuki. Ungana nasi.
23.10.2024 Matangazo ya Jioni
Mkutano wa 16 wa kilele wa Jumuiya ya BRICS unaendelea mjini Kazan nchini Urusi//Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili mjini Riyadh nchini Saudi Arabia// Ijumaa ni siku ya mwisho kwa umma huko Kenya kuwasilisha maoni yao kuhusu muswada tata unaotaka kuongeza muda wa kuhudumu wa rais pamoja na viongozi wengine wa kisiasa waliochaguliwa kama vile wabunge kutoka miaka 5 hadi 7.
BRICS yataka vita vikomeshwe Gaza, Ukraine
BRICS inaharakisha mfumo mbadala wa malipo katika biashara ya kimataifa kuuepuka mfumo wa Magharibi.
23.10.2024 Matangazo ya Mchana
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amewasili Urusi kuhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS, ziara yake ya kwanza nchini humo baada ya zaidi ya miaka miwili,//Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema 'sasa ni wakati' wa kuvimaliza vita vya Gaza
23.10.2024 Matangazo ya Asubuhi
Naibu Rais Rigathi Gachagua atasubiri kiasi kufahamu hatma yake// Mkutano wa 16 wa kilele wa jumuiya ya BRICS ulianza jana mjini Kazan nchini Urusi. Mkutano huo unatarajiwa kupitisha maazimio muhimu sana juu ya ushirikiano wa kifedha utakaokwepa mfumo wa kifedha wa ulimwengu unaotawaliwa na Marekani// Zaidi ya wiki mbili zikiwa zimebakia kabla ya uchaguzi wa rais nchini Marekani.
Mwangaza wa Ulaya: Athari za utalii uliokithiri Barcelona
Jiji la Uhispania la Barcelona ni lenye historia ya kipekee, hali ya hewa ya joto na fukwe za kupendeza. Lakini sifa zote hizi zimeifanya Barcelona kuwa kivutio kwa mamia ya maelfu ya wageni na hivyo kuathirika na viwango vya juu vya utalii. Idadi ya watalii wanaoutembelea mji huo inazidi kuongezeka na hivyo kuchochea hasira miongoni mwa wenyeji wanaolalamika kwamba mambo mengi yamebadilika.
23.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Israel imethibitisha kumuua kiongozi wa Hezbollah aliyetazamiwa kuchukua nafasi ya Hassan Nasrallah. Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya BRICS inaingia katika siku yake ya pili hivi leo huko Kazan, nchini Urusi. Watu 11 wafariki nchini Uganda baada ya lori la mafuta kupata ajali na kuripuka.
Modi amuambia Putin afanye mazungumzo na Zelensky
Putin anaendelea kukutana na viongozi mbalimbali tayari wanaohudhuria mkutano wa 16 wa kilele wa jumuiya ya BRICS.
22.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Kenya Wiliam Ruto amesema mahakama inayoisikiliza rufaa ya naibu wa rais aliyeondolewa madarakani Rigathi Gachagua haina mamlaka ya kuendesha kesi hiyo+++Rais Vladimir Putin wa Urusi anaendelea kuwapokea na kukutana na viongozi mbalimbali wa dunia kwa ajili ya mkutano wa 16 wa kilele wa jumuiya ya BRICS unaofanyika mjini Kazan.
22.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Israel kuendeleza hatua zaidi za kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza+++Wapiganaji wa kundi la RSF la Sudan wamesema wameidungua ndege ya mizigo magharibi mwa Darfur.
22.10.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Wapiganaji wa kundi la M23 wamefanikiwa kuudhibiti mji wa Kalembe wilayani Masisi na kusonga mbele hadi wilaya jirani ya Walikale mkoani Kivu Kaskazini+++Wakuu wa mashirika ya fedha duniani watakusanyika mjini Washington Marekani wiki hii huku kukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya vita katika Mashariki ya Kati na Ulaya.
22.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Israel yashambulia karibu maeneo 300 ya Hezbollah. Uingereza kuipatia Ukraine mkopo wa dola bilioni 2 kukabiliana na uvamizi wa Urusi. Uganda yawatia hatiani kwa "uhaini" wanachama 16 wa upinzani.
21.10.2024 Matangazo ya Jioni
Kundi la Hezbollah limesema limewashambuliwa wanajeshi wa Israel Kusini mwa Lebanon// Wapigakura nchini Moldova wameridhia kwa wingi mdogo kujiunga na Umoja wa Ulaya// Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia Wakimbizi Filippo Grandi ameanza ziara ya wiki moja Uganda
Dana Dana za Bundesliga na Bruce Amani
VfB Stuttgart si imara sana msimu huu kulinganisha na jinsi ilivyocheza msimu uliopita.
Mechi za ligi ya mabingwa Champions kuendelea wiki hii
Bayern Munich watakuwa ugenini kukipiga na Barcelona.
Bayern na Leipzig zakabana koo katika Bundesliga
Aryana Sabalenka na Iga Swiatek wachuana kuwania nafasi ya mchezaji bora wa tenis msimu huu.
21.10.2024 Matangazo ya Mchana
Wapiganaji wa kundi la M23 wameuteka tangu hapo jana Jumapili mji muhimu wa Kalembe wilayani Masisi// Naibu wa Rais wa Kenya aliyeondolewa madarakani Rigathi Gachagua amemkosoa vikali Rais William Rutto na kumuita mtu katili// Uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania imekamilika rasmi uku baadhi ya vyama vya upinzani vikilalamika.
21.10.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
21.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Marekani yataja kuendeleza juhudi za kuvimaliza vita vya Mashariki ya Kati. Urusi kuwa mwenyeji wiki hii wa mkutano wa kilele wa BRICS. Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya M23 na wanamgambo wanaojiita Wazalendo
Ufaransa yaiunga mkono Ukraine mpango wa kukomesha vita
Ufaransa inasema inauunga mkono mpango wa Ukraine wa kuvimaliza vita vya miaka miwili na nusu kati yake na Urusi.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Kenya ilimpata Naibu mpya wa Rais ambaye ni Kithure Kindiki baada ya Baraza la Seneti kuidhinisha kutimuliwa madarakani kwa Rigathi Gachagua. Lakini Mahakama Kuu nchini humo ilisitisha mchakato mzima hadi Oktoba 24. Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unapinga vikali hatua ya chama tawala UDPS kuanzisha mchakato wa kubadili katiba. Kwa hayo na mengine, ungana na Bakari Ubena.
18.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Spika wa bunge la taifa nchini Kenya amelichapisha rasmi jina la naibu wa rais mteule Kithure Kindiki kwenye gazeti rasmi la serikali. Wakati huohuo, mahakama kuu imesitisha kwa muda kuondolewa kwa Rigathi Gachagua kwenye nafasi yake ya unaibu rais+++Kundi la wanamgambo wa Hamas limethibitisha kifo cha kiongozi wake Yahya Sinwar, aliyeuliwa na wanajeshi wa Israel.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Matukio ya barani Afrika yaliyozingatiwa na magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii ni pamoja na idadi yinayoongezeka ya wakimbizi kutoka jimbo la Darfur wanaoelekea nchini Chad. Juu ya kuongezeka maambukizi ya mpox kwenye nchi kadhaa za Afrika. Je yuko wapi Rais Paul Biya wa Cameroon? Mtayarishaji, Zainab Aziz.
18.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Rais William Ruto wa Kenya amemteua Profesa Kindiki Kithure kuwa Naibu wake, siku moja tu baada ya Bunge la Seneti kumvua madaraka Rigathi Gachagua+++Rais Joe Biden wa Marekani ambae kwa hivi sasa yupo mjini Berlin, Ujerumani, tayari amekutana na mwenyeji wake, Rais Frank-Walter Steinmeier, katika Kasri la Bellevue
18.10.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Naibu wa rais Rigathi Gachagua atimuliwa na baraza la Senate+++Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani, kama ambavyo amekuwa akifanya kwa miongo kadhaa.
17.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Mawakili wanaomuwakilisha Naibu wa Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua katika kesi ya kuondolewa kwake madarakani wameondoka katika bunge la seneti leo huku vikao vikiendelea+++Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeripoti kuwa zaidi ya watu bilioni moja wanaishi katika umaskini mkubwa duniani kote
17.10.2024 - Matangazo ya Mchana
Israel imefanya mashambulizi Gaza, Lebanon na Syria huku mshirika wake mkuu Marekani ikishambulia ngome za waasi wa Kihouthi nchini Yemen+++Viongozi wa Mataifa ya Ghuba, ikiwa ni pamoja na Mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman walikutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels katika mkutano wa kwanza wa kilele baina ya pande hizo
17.10.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Meya wa mji wa Freetown nchini Sierra Leone, Yvonne Aki-Sawyerr, ndiye mshindi wa Tuzo ya Ujerumani kwa Afrika kwa mwaka 2024+++Serikali ya Tanzania imesema sehemu kubwa ya taarifa iliyotolewa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua kuondoa hali ya kuzorota kwa hali ya haki za binadamu zimetiwa chumvi.
16.10.2024 Matangazo ya Jioni
Uingereza, Ufaransa na Algeria wametoa wito wa mkutano wa dharura kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hali ya kiutu katika Ukanda wa Gaza / Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema mamilioni ya watu Kusini mwa Afrika wanakabiliwa na njaa
16.10.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Baraza la Senate limeanza mchakato wa kusikiliza tuhuma zinazonuwia kumtimua naibu wa rais Rigathi Gachagua, nchini Kenya / Jeshi la Israel lashambulia tena mji wa Beirut
15.10.2024 - Matangazo ya Jioni
Mahakama nchini Kenya imetupilia mbali ombi la Naibu Rais Rigathi Gachagua la kuitaka kusitisha kesi yake iliyopangiwa kuanza kusikizwa kesho katika bunge la Seneti+++Taifa Stars ya Tanzania imepoteza mechi yake ya kufuzu kwa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2025 nchini Moroko kwa kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa DR Kongo
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 128
Ukurasa unaofuatia