1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU na EU zaongeza shinikizo kwa viongozi wa mapinduzi Niger

Sylvia Mwehozi
29 Julai 2023

Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, umeongeza shinikizo kwa viongozi wa mapinduzi nchini Niger na kutaka kurejeshwa utawala wa kikatiba.

https://p.dw.com/p/4UXZ5
Screenshot DW Sendung Niger
Picha: DW

Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, umeongeza shinikizo kwa viongozi wa mapinduzi nchini Niger na kutaka kurejeshwa utawala wa kikatiba. Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika, limewataka wanajeshi kurejea mara moja na bila masharti katika kambi zao ndani ya muda usiozidi siku kumi na tano.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lalaani mapinduzi ya Niger

Naye mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema hawatotambua utawala wa kimapinduzi na kutangaza kusitisha ushirikiano wa kiusalama na Niger. Borrell ameongeza kuwa wako tayari kuunga mkono hatua zitakazochukuliwa na Jumuiya ya kikanda ya ECOWAS ikiwemo uanzishwaji wa vikwazo.

Viongozi wa ECOWAS wanakutana kesho mjini Abuja kujadili mapinduzi hayo amesema Rais Bola Tinubu wa Nigeria. Wakati huo huo pia Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amefanya mkutano na maafisa wake wa ulinzi kuhusu mapinduzi ya Niger.