Macron kuongoza mkutano wa ulinzi kuhusu mapinduzi ya Niger
29 Julai 2023Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa ofisi ya rais huyo. Macron amelaani vikali hatua ya waasi hao ya kumuondoa madarakani Mohamed Bazoum siku ya Jumatano.
Soma zaidi: Jenerali Abdourahamane Tiane ajitangaza kuwa kiongozi mpya Niger
Kiongozi huyo wa Ufaransa amesema mapinduzi hayo ya kijeshi ni haramu na ni hatari kwa watu wa Niger, na eneo zima kwa ujumla huku akitoa wito wa kuachiwa huru kwa Bazoum na kudumishwa kwa utaratibu wa kikatiba.
Ufaransa ina takriban wanajeshi 1,500 katika taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo ni moja ya washirika wake wa mwisho katika eneo la Sahel, baada ya vikosi vyake kuondoka katika nchi jirani ya Mali mapema mwaka huu.