Mke na mume wafungwa zaidi ya miaka 30 kwa mauaji ya mtoto
18 Desemba 2024Urfan Sharif, mwenye umri wa miaka 43, amehukumiwa kifungo cha miaka 40, huku mkewe Beinash Batool, mwenye umri wa miaka 30, akihukumiwa kifungo cha miaka 33 kwa mauaji yaSara Sharif. Mahakama hiyo ilielezwa kuwa mwili wa Sarah ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa akiwa amevujika baadhi ya viungo vya mwili pamoja na kuwa na majeraha ya kuchomwa na pasi. Jaji John Cavanagh amesema Sarah alikuwa muathirika wa mateso ya kupitiliza na kwamba Sharif na Batool hawakuonesha dalili zozote za kujutia matendo yao. Alikutwa akiwa amekufa kitandani mwake mwezi Agosti mwaka 2023 akiwa peke yake nyumbani. Uchunguzi wa maiti umeonyesha kuwa Sara alikuwa na majeraha 71 na kuvunjika mifupa mara 25. Mjomba wake, Faisal Malik, aliye na umri wa miaka 29, pia alipatikana na hatia ya kusaidia au kuruhusu mauaji hayo kutokea na amehukumiwa kifungo cha miaka 16.