Baraza la Usalama latoa wito wa kusimamisha mapigano Sudan
24 Juni 2023Matangazo
Taarifa hiyo fupi kwa vyombo vya habari ilitolewa baada ya mashauriano ya faragha. Baraza hilo pia limetaka kuongezwa kwa misaada ya kibinadamu kwa Sudan na kwa nchi jirani. Pia limetoa wito wa kuwaunga mkono wafanyakazi wanaogawa misaada na linataka sheria za kimataifa ziheshimiwe.
Soma zaidi:Wasudan waendelea kushambuliana licha ya makubaliano
Sudanilitumbukia katika mzozo katikati ya mwezi Aprili baada ya miezi kadhaa ya kuongezeka mivutano iliyosababisha mapigano ya wazi kati ya majenerali mahasimu. Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa tangu kuanza kwa vita hivyo, watu milioni 2.8 nchini Sudan wamepatiwa misaada muhimu na shirika hilo.