Baraza la Usalama laonya dhidi ya hali mbaya Kongo
21 Juni 2024Baraza hilo limesema mashambulizi ya waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) yamekuwa yakiongezeka kwenye eneo hilo.
Vile vile limelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya M23, ambayo vyanzo vya ndani vinasema yalikuwa ya umwagaji mkubwa wa damu.
Soma zaidi: AU walaani mauaji ya watu wengi nchini DR Congo
Mashambulizi ya wiki iliyopita huko Kanyabayonga, mji muhimu katika eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye machafuko, yaliwafanya watu 350,000 kupoteza makaazi yao.
Ingawa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikulitaja bayana jina la Rwanda, lakini lililaani kile ilichokiita msaada wa kijeshi wa kigeni unaotolewa kwa waasi na kutoa wito wa kuondolewa mara moja kwa vikosi vyote vya kigeni.
Rwanda imekuwa mara kadhaa ikikanusha kuwaunga mkono waasi wa M23.