Bazoum akanusha kutaka kutoroka Niger
20 Oktoba 2023Matangazo
Mratibu wa kundi la wanasheriahao, Mohamed Seydou Diagne, amesema katika taarifa waliyoitoa Ijumaa (Oktoba 20) kuwa wanapinga vikali shutuma hizo za uzushi dhidi ya Rais Bazoum.
Wakili huyo alisisitiza kwamba utawala wa kijeshi umevuuka mstari mwekundu kwa kumshikilia rais huyo sehemu kusikojulikana na kwamba hilo linakiuka haki zake za msingi.
Soma zaidi: Viongozi wa kijeshi wa Niger wadai kuzima jaribio la Bazoum kutoroka
Tangu apinduliwe madarakani Julai 26, Bazoum amekataa kujiuzulu rasmi na hivyo kuendelea kuzuiliwa pamoja na familia yake.
Mwezi Septemba, mawakili wake waliwasilisha shauri katika Mahakama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) dhidi ya wanajeshi waliompindua Rais Bazoum.