1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Dunia: Hasara ya tetemeko la ardhi $ 5.1 bilioni

4 Machi 2023

Benki ya Dunia imesema kuwa tetemeko la ardhi la mwezi Februari limesababisha uharibifu wa moja kwa moja unaokadiriwa kuwa bilioni 5.1 nchini Syria.

https://p.dw.com/p/4OFcl
Erdbeben
Picha: Rami Alsayed/dpa/picture alliance

Tetemeko la ardhi lililotokea Februari 6 nchini Uturuki na Syria limeharibu miji na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50,000 katika nchi hizo mbili.

Taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa (Machi 3) na Benki ya Dunia ilieleza kuwa mamilioni ya watu wameachwa bila msaada wa dharura wa makaazi na huduma ya afya.

Soma zaidi: Misri imeahidi "mshikamano na huruma" kwa Syria
Ujerumani yaahidi misaada zaidi kwa Uturuki na Syria

Uharibifu huo umeyaathiri zaidi majimbo manne, ambako takribani watu milioni 10 wa Syria wanaishi.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, jimbo lililoathirika zaidi ni Aleppo, ambalo limeharibiwa kwa asilimia 45, likifuatiwa na majimbo ya Idlib na Lattakia.

Mwezi uliopita, Benki ya Dunia ilisema tetemeko hilo la ardhi limesababisha uharibifu wa moja kwa moja Uturuki, wa dola bilioni 34.2.