1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ulaya ya Magharibi yakosa umeme usiku

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvp

Sehemu fulani za Ufaransa yakiwemo maeneo ya mji mkuu wa Paris zimekuwa kizani wakati wa usiku kutokana na kukatika kwa umeme kulikodumu kwa dakika 90.

Miji mitatu ya Ujerumani pia ilikumbwa na kukatika huko kwa umeme.Kampuni ya nishati ya Ujerumani RWE imesema hali ya hewa ya baridi imesababisha kukatika huko kwa umeme karibu katika Ulaya yote ya magharibi.

Jana usiku kulikuwa na ongezeko la mahitaji ya umeme wakati viwango vya baridi vilipoongezeka kufikia hali ya kuganda kwa barafu.

Kuaminika kwa mfumo wa umeme barani Ulaya kumekuwa kukidhoofishwa katika miaka ya hivi karibuni wakati mahitaji ya umeme yakiongezeka na uwekezaji katika uzalishaji zaidi wa umeme ukiwa hauoani na mahitaji.