Biden aeleza wasiwasi kuhusu mgogoro wa kisiasa bungeni
5 Oktoba 2023Matangazo
Bunge la Marekani linatarajiwa kuidhinisha bajeti ya mwaka ujao mnamo kipindi cha mwezi mmoja na nusu.
Marekani inatumai kwamba bajeti hiyo itajumuisha pia msaada mpya wa dola bilioni 24 kwa ajili ya Ukraine.
Ofisi ya rais Biden imesema fedha hizo zinahitajika katika kuendelea kuiunga mkono Ukraine ili iweze kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
Hata hivyo, utawala wa Biden unakabiliwa na tatizo kubwa kutokana na wabunge wahafidhina wanaopinga vikali msaada kwa ajili ya Ukraine jambo lililochangia pia kuondolewa kwenye wadhifa, Spika wa bunge Kevin McCarthy.