1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden kukutana na Netanyahu katika Ikulu ya White House

23 Julai 2024

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Alhamisi katika Ikulu ya White House. Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4ic35
Marekani | Joe Biden | Rais wa Marekani Biden na Benjamin Netanyahu 2023
Biden na Netanyahu wanatajadili njia za kusitishwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa HamasPicha: Evelyn Hockstein/File Photo/REUTERS

Biden amekuwa akipambana na ugonjwa wa UVIKO-19 tangu Jumatano iliyopita lakini anarejea Washington Jumanne akitokea kwenye makazi yake ya ufukweni huko Delaware. Netanyahu atahutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani Jumatano.

Biden na Netanyahu wanatarajiwa kujadili njia za kupatikana makubaliano ya kusitishwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, pamoja na Iran na mada nyingine.

Soma pia: Rais Biden asitisha kampeni baada ya kugundulika na UVIKO

Utakuwa mkutano wa kwanza wa Biden na kiongozi wa kigeni tangu alipojiondoa katika mbio za urais na kumpendekeza Makamu wa Rais Kamala Harris kuwa mrithi wake kama mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic. Harris atakutana na Netanyahu wiki hii katika mkutano tofauti na wa Biden.