1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kukutana na viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya

20 Oktoba 2023

Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kuwapokea kwa mazungumzo katika Ikulu ya White House, Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, na Rais wa Baraza la Umoja huo, Charles Michel.

https://p.dw.com/p/4Xmo8
Washington White House Biden Rede Israel Ukraine
Rais Joe Biden wa Marekani.Picha: Jonathan Ernst/AFP

Mazungumzo hayo muhimu mjini Washington yanatazamiwa kujikita kwenye vita vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. 

Soma zaidi: EU yaungana kuhusu Ukraine, lakini haitatoa uanachama wa haraka

Biden na viongozi hao wa Ulaya watajadili pia masuala ya ushirikiano katika masuala ya teknolojia ya akili bandia, miundombinu ya kidijitali pamoja na sera ya biashara.

Ulaya na Marekani zimekuwa katika mvutano kuhusu ushindani wa kibiashara katika sekta mbalimbali.