1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLANTYRE:Shutuma za rushwa dhidi ya rais wa zamani wa Malawi.

19 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEQI

Afisa mmoja mwandamizi kutoka chama cha tawala cha zamani nchini Malawi,ameliambia Bunge la nchi hiyo kuwa aliyekuwa Rais wa Malawi Bwana Bakili Muluzi,alihamishia katika akaunti yake dola milioni 12 zilizochangwa kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi wa mwaka jana.

Afisa huyo mwandamizi kutoka chama cha United Democratic Front-UDF,George Mtafu ambaye ni kiongozi wa chama hicho bungeni,amesema hata hivyo chini ya sheria za Malawi sio dhambi kupokea fedha za michango na linakuwa kosa iwapo fedha hizo ni mali ya umma.

Mtafu ambaye ni mtu wa karibu sana na Bwana Muluzi,alikuwa akielezea hayo baada ya kitengo cha kupambana na ruswa nchini humo,kumfanyia uchunguzi Muluzi kwa tuhuma za rushwa inayohusisha mamilioni ya dola,fedha zilizopokelewa kutoka Taiwan,Libya,Morocco na nchi nyingine.

Mtafu ameonesha wasiwasi wake kuwa kuna dhamira ya dhati ya kupekua akaunti binafsi na hivyo kumsababishia usumbufu rais huyo wa zamani wa Malawi.

Shutuma za rushwa dhidi ya Muluzi zimekuja baada ya chama chake bungeni kushupalia kumshtaki Rais wa sasa Bingu wa Mutarika kwa tuhuma za kukiuka katiba.