1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Blinken awasili Israel kwa duru nyingine ya mazungumzo

7 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Israel kwa duru nyingine ya mazungumzo ambayo yanalenga kufikia usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4c8j6
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Rais wa Israel Isaac Herzog mjini Jerusalem mnamo  Februari 7, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) na Rais wa Israel Isaac Herzog (kulia)Picha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Blinken alikutana kwanza na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem siku moja baada ya mazungumzo nchini Qatar, ambayo ilisimamia makubaliano yanayoripotiwa kuwa ya awamu ambayo yatailazimu Israel kusitisha operesheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza na kuachiliwa huru kwa mateka wake kutokaGaza na pia wafungwa wa Kipalestina kutoka Israel.

Hii ni kulingana na vyanzo vya Marekani.

Blinken akutana na Rais wa Israel Isaac Herzog

Baada ya mkutano huo, Blinken pia alikutana na rais wa nchi hiyo Isaac Herzog mjini Jerusalem.

Wakati wa mkutano huo,Blinken alitoa wito mpya wa msaada kuelekea Gaza na kuongeza kuwa kuna wanaume, wanawake na watoto wengi wasiokuwa na hatia wanaopata mateso kutokana na mapigano hayo.

Soma pia: Blinken amuhimiza Netanyahu kuruhusu misaada Gaza

Blinken ameongeza kusema kwamba wote wana jukumu la kufanya kila linalowezekana kupata msaada unaohitajika ili uweze kufikishwa kwa wale wanaouhitaji zaidi na hatua zinazochukuliwa, hatua za zaidi zinazohitaji kuchukuliwa, ndilo lengo la mikutano yake katika eneo hilo.

Blinken pia ameelezea matumaini ya kupatikana kwa makubaliano ya kuanza kuwaachiwa huru tena kwa mateka wa Israel kutoka Gaza lakini akasema kazi zaidi inahitajika kufanywa .

Kikosi cha Israel chafyatua risasi kuelekea Gaza, Februari 4, 2024 wakati mzozo ukiendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza
Kikosi cha Israel chafyatua risasi kuelekea GazaPicha: Dylan Martine/REUTERS

Maafisa wa Israel wamesema kuwa wanatazama kwa makini pendekezo jipya la usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza lililowasilishwa na wapatanishi wa Qatar. Haya yamesemwa leo na msemaji wa serikali wa nchi hiyo Avi Hyman .

Soma pia: Blinken azungumza na Israel juu ya pendekezo la Hamas

Hyman amewaambia wanahabari kwamba wamepokea pendekezo hilo kutoka kwa wapatanishi hao wa Qatar na kwamba wanalifanyia tathmini, akirudia taarifa ya jana jioni.

Wahanga wa Ufaransa wakumbukwa katika sherehe ya kitaifa

Raia 42 wa Ufaransa waliofariki katika shambulio la kushtukiza la Hamas dhidi ya  Israel pamoja na mateka watatu ambao bado wanaaminika kushikiliwa na kundi la Hamas linachokuliwa kuwa la kigaidi na Israel pamoja na washirika wake, wamekumbukwa na kutolewa heshima wakati wa sherehe hiyo ya kitaifa iliyofanyika nchini Ufaransa. 

Soma pia: Blinken awasili Mashariki ya kati kwa mara ya tano

Viti vitatu vitupu vilivyoashiria kutokuwepo kwao, viliwekwa karibu na familia za wahasiriwa waliohudhuria hafla hiyo.

Rais Macron amesema kwamba wale waliouawa ''hawatawahi kutimiza miaka 30'' huku akikemea kile alichokiita ukatili unaozingatia chuki dhidi ya wayahudi na kuenezwa kwake.

Macron amesema kuwa Ufaransa itaendelea kujizatiti kuafikia matarajio ya amani na usalama katika Mashariki yote ya Kati.