Blinken kuhudhuria mkutano kuhusu Haiti
11 Machi 2024Mkutano huo unafanyika wakati shinikizo la kumtaka Waziri Mkuu Ariel Henry ajiuzulu au akubali kuunda baraza la mpito.
Henry, ambaye amezuiwa kurejea nchini mwake baada ya kuongezeka kwa machafuko, alitarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa faragha siku ya Jumatatu (Machi 11).
Soma zaidi: CARICOM yawaalika wanadiplomasia wa mataifa makubwa kuijadili Haiti
Mkutano huo uliandaliwa na wanachama wa Jumuiya ya Kibiashara ya Karibiani (CARICOM), ambayo kwa miezi kadhaa imekuwa ikishinikiza kuundwa kwa serikali ya mpito nchini Haiti, huku waandamanaji wakimtaka Henry ajiuzulu.
Henry aliwasili nchini Puerto Rico wiki iliyopita baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia Jamhuri ya Domikani, taifa jirani la Haiti.
Tayari balozi za kigeni zimewahamisha wafanyakazi wake kutoka mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, kufuatia machafuko ya magenge ya wahalifu yanayosambaa katika mji huo.