Blinken, Stoltenberg waonya mafanikio ya Ukraine
30 Januari 2024Akizungumza katika kikao cha pamoja cha waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg mjini Washington, Blinken amesema kuwa bila kutolewa fedha hizo za nyongeza, Marekani itakuwa inatuma ujumbe mzito na usio sahihi kwa maadui wake wote kuwa haiko makini kuhusu kuutetea uhuru, na kuitetea demokrasia.
Biden ameliomba bunge la Congress kuidhinisha dola bilioni 61 kama msaada mpya kwa Ukraine. Stoltenberg atakutana leo na wabunge ili kueleza jinsi hali ilivyo Ukraine.
Soma pia:Ukraine yataka uchunguzi wa kimataifa katika ajali ya ndege ya Urusi
Wabunge wa Republican wanasita kuendelea kuifadhili Kyiv, wakisema haina mkakati wa wazi wakati mapigano dhidi ya wanajeshi wa Rais wa Urusi Vladmir Putin yakiendelea.
Stoltenberg amesema kama Putin atashinda vita, itakuwa ni janga sio tu kwa Ukraine bali pia itafanya ulimwengu kuwa hatari zaidi na kila mmoja kukosa usalama.