1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa 65 wa kivita wafa baada ya ndege ya Urusi kuanguka

24 Januari 2024

Gavana wa jimbo la Urusi la Belgorod amethibitisha kwamba watu wote waliokuwamo katika ndege ya kijeshi ya mizigo wamekufa baada ya kuanguka katika jimbo hilo.

https://p.dw.com/p/4bd8h
Moto ukizuka kwenye eneo ilipoanguka ndege ya kijeshi ya Urusi.
Moto ukizuka kwenye eneo ilipoanguka ndege ya kijeshi ya Urusi.Picha: UGC/AP/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema mapema kwamba watu 74 walikuwamo kwenye ndege hiyo ikiwa pamoja na wafungwa wa kivita 65 wa Ukraine.

Mateka hao waliopaswa kuachiwa kwa kubadilishana na mateka wa vita wa Urusi.

Kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Belgorod, muda mfupi kabla ya ndege hiyo kuanguka, tahadhari juu ya kombora ilitolewa na kuwataka watu wajibanze kwenye  sehemu salama.

Wakati huo huo, taarifa kutoka makao makuu ya kuratibisha wafugwa wa kivita nchini Ukraine imesema utafanyika uchunguzi wa mkasa wa kuanguka ndege hiyo.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na badala yake watu wametahadharishwa juu ya kupeana taarifa ambazo hazijathibitishwa.