1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Vita vya Gaza: Antony Blinken ziarani Mashariki ya Kati

8 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken anatarajiwa hii leo kufanya mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Saudi Arabia katika juhudi zake za kutuliza mzozo katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4axW5
Griechenland Abflug US Außenminister Blinken nach Jordanien
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken akiwasili mjini Amman nchini Jordania: 06.01.2024Picha: Evelyn Hockstein/AFP

Baadaye Blinken ataelekea Israel na katika ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni ziara yake ya nne katika eneo la Mashariki ya Kati katika kipindi cha miezi mitatu. Serikali mjini Tel-Aviv imeapa kuendelea na vita vyake huko Gaza hadi itakapolitokomeza kabisa kundi la Hamas.

Akiwa mjini Doha nchini Qatar, Blinken amesisitiza  umuhimu wa Israel kubadili operesheni zake za kijeshi kupunguza wahanga wa kiraia na kuimarisha kwa kiwango kikubwa upelekaji wa misaada ya kiutu huko Gaza, huku akionya kuwa vita hivyo vinaweza kutanuka katika eneo zima la Mashariki ya Kati endapo hakutakuwa juhudi za amani.