Bunge la Kenya lapokea hoja ya kuuzuliwa makamu wa rais
1 Oktoba 2024Matangazo
Maelezo hayo yametolewa na spika wa bunge la nchi hiyo, wakati vyambo vya habari vya Kenya vikiripoti kwamba makamu huyo wa rais amekosana na Rais William Ruto.
Zaidi ya thuluthi moja ya wabunge wamesaini hoja hiyo iliyowasilishwa na mbunge Mwengi Mutuse anayeegemea kambi ya muungano wa Rais Ruto.
Soma zaidi: Gachagua: Idara ya Ujasusi yaifelisha serikali ya Kenya
Muungano huo unamtuhumu Gachagua, miongoni mwa mambo mengine, kwamba anawanyima watu fursa za kupata uteuzi wa nafasi za umma na rasilimali.
Mpasuko kati ya Ruto na Gachagua umekuwa ukionekana waziwazi katika siku za hivi karibuni nchini Kenya, huku makamu huyo wa rais akisema ametengwa katika shughuli za kiserikali.