Burkina Faso ni adui wa sera za Ufaransa, si watu wake
7 Septemba 2023Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha serikali cha RTB, Traore amesema, sera za wanaoiongoza serikali ya Ufaransa ni tatizo barani Afrika.
Ameongeza kwamba nchi hazina budi kukubali kuwa na usawa na kwamba haoni tatizo ikiwa serikali hazitakuwa na mitizamo ya kibeberu.
Soma zaidi: Burkina Faso yafukuza waandishí habari wa magazeti ya Ufaransa
Traore bila kutoa maelezo ya kina amesema, wapo watu waliopelekwa kutia saini mikataba mingi inayozuwia maendeleo. Ametanabaisha kwamba Ufaransa si taifa pekee la kibeberu bali yako pia mataifa mengine.
Kiongozi huyo wa kijeshi wa Burkina Faso alingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 2022 na baada ya hapo, Ufaransa iliwaondoa wanajeshi wake baada ya uhusiano kati ya mataifa hayo mawili kuzorota.