1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya 8 ya Mataifa ya Afrika kuanza Februari Mosi

17 Septemba 2024

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe ametangaza jana kwamba michuano ya nane ya Mataifa ya Afrika itafanyika kuanzia Februari 1 hadi 28 nchini Kenya, Tanzania na Uganda.

https://p.dw.com/p/4khBH
Patrice Motsepe
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF Patrice Motsepe ametangaza tarehe rasmi ya kuanza michuano ya Mataifa ya Afrika Picha: Weam Mostafa/Sports Inc/empics/picture alliance

Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuandaa mashindano ya kandanda ya timu za taifa. Motsepe alizuru viwanja vitatu vya taifa nchini Kenya vilivyotengwa kwa ajili ya michuano hiyo, na kusema ameridhishwa na dhamira iliyoonyeshwa na nchi hizo tatu.

Mechi za kufuzu kushiriki michuano hiyo itakayoshirikisha timu 19 zitaanza Oktoba 25 na kumalizika mwezi Disemba.

Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, zimeshinda mara mbili kombe la michuano hii inayohusisha wachezaji wa ndani, CHAN tangu ilipoanzishwa 2009.