CHADEMA waandamana Dar es Salaam
24 Januari 2024Matangazo
Maandamano hayo ni ya kuishikiniza serikali kuondoa bungeni miswada mitatu ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi na kuboresha katiba mpya, pamoja na mambo mengine.
Mbowe, pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA, Godbless Lema, Benson Kigaila na Joseph Mbilinyi waliongoza msafara wa waandamanaji hao waliokuwa wameshika bendera za chama hicho na mabango yenye jumbe mbalimbali.
Jeshi la polisi lilitoa kibali cha kuwaruhusu kufanya maandamano hayo na kuahidi kuyasimamia.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mji wa Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alifika eneo la Buguruni mapema asubuhi na kuanza kuongoza misafara ya pikipiki na magari kabla ya maandamano hayo kuanza.