1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China inaweza kuwa muwezeshaji, sio mpatanishi Ukraine

31 Machi 2023

Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borell amesema China haiwezi kuwa mpatanishi katika vita vya Ukraine kwa kuwa inaegemea zaidi upande wa mvamizi ambaye ni Urusi

https://p.dw.com/p/4PZE1
Belgien EU-Verteidigungsaußenminister
Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP Photo/picture alliance

Borell, mkuu wa masuala ya kigeni wa umoja huo amesema hata hivyo China inaweza kuchukua dhima ya mwezeshaji kwa ajili ya kupatikana makubaliano ya amani na Urusi.

Soma pia: Ukraine itaamuwa kuhusu mahusiano ya China na Umoja wa Ulaya: Ursula

Borell aliyekuwa akizungumza katika mji mkuu wa Uhispania, Madrid, amesema mpango wa amani wa pekee ni ule uliowasilishwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy mwezi Novemba, uliotaka Urusi iviondoe vikosi vyake na kurudisha maeneo iliyoyateka kabla ya kuizingira Crimea mwaka 2014.

Matamshi hayo ya Borell yanaunga mkono wito wa Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez aliutoa kwa Rais wa China Xi Jinping, wa kumtaka azungumze na Zelenskiy na ajifahamishe kuhusu mpango wa amani wa Ukraine.