1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaanza luteka ya siku tatu kuzunguka Taiwan

8 Aprili 2023

China inafanya luteka kubwa ya kijeshi kuanzia kuzunguka Taiwan katika kile serikali mjini Beijing imesema kuwa ni "onyo kali" kwa utawala wa kisiwa hicho baada ya rais wake kukutana na spika wa bunge la Marekani.

https://p.dw.com/p/4PptF
Meli ya kivita ya China
Mieli ya kivita ya China ikipita karibu na kisiwa cha Taiwan katika siku ya kwanza ya luteka ya kijeshi Picha: Thomas Peter/Reuters

Luteka hiyo ya siku tatu iliyopewa jina la "upanga wa ncha kali" inajumuisha makumi ya meli na ndege za kivita zitakazofanya mazoezi ya kijeshi upande wa mashariki na kaskazini mwa Taiwan.

Onesho hilo la nguvu za kijeshi linafuatia mkutano ulioikasirisha China ambao uliwakutanisha rais Tsai Ing-wen wa Taiwan na spika wa  bunge la Marekani Kevin McCarthy huko mjini California

Rais Tsai amelaani mazoezi hayo ya kijeshi kuzunguka Taiwan , kisiwa ambacho China inakizingatia kuwa sehemu ya himaya yake na imeapa siku moja itakirejesha chini ya milki yake.