1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaendeleza luteka za kijeshi kuizunguka Taiwan

10 Aprili 2023

Ndege na meli za kivita za China zimeendelea na mazoezi ya kijeshi kukizunguuka kisiwa cha Taiwan inachokichukulia kama semehu ya himaya yake.

https://p.dw.com/p/4Prvj
China startet dreitägige Militärübungen rund um Taiwan
Picha: Eastern Theatre Command/REUTERS

Ndege na meli za kivita za China zimeendelea na mazoezi ya kijeshi kukizunguuka kisiwa cha Taiwan inachokichukulia kama semehu ya himaya yake.

China inafanya mazoezi hayo ikiwa ni kujibu mkutano wa Rais wa Taiwan Tsai Ing-Wen na Spika wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy.

Soma zaidi: China yaanza luteka ya siku tatu kuzunguka Taiwan
China yamuwekea vikwazo Balozi wa Taiwan na taasisi za Marekani

Operesheni hiyo ya siku tatu ya China iliyopewa jina la "Upanga wa Pamoja" kukizunguuka kisiwa hicho, leo Jumatatu itahusisha mazoezi ya kuzima moto kwenye pwani ya miamba katika mkoa wa Fujian nchini China ikiwa ni takriban kilometa 190 kutoka Taipei.

Mazoezi hayo yameshutumiwa vikali na Taipei na kutoa wito wa kujizuia huku Washington ikisema "inafuatilia kwa ukaribu vitendo vya Beijing."